Kenya yawapiga Al Shabaab

Kenya
Image caption Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta na naibu rais William Ruto

Jeshi la Kenya limesema kuwa wameua wapiganaji 57 wa kundi la kigaidi la Al Shabaab katika mapambano huko kusini mwa Somalia mapema wiki hii. (Jumatano)

Waziri wa ulinzi wa Kenya amesema kuwa Vikosi chini ya majeshi ya umoja wa Africa (amisom) vilitumia mashmbulizi ya anga dhidi ya waasi hao karibu na mji wa Afmadow, takribani kilometa 100 kaskazini magharibi mwa Kismayo.

Lakini Al-Shabaab walikana juu ya taarifa hiyo ya kuuawa kwa wapiganaji wake.