Shakira ashtakiwa kwa wizi wa Wimbo

Shakira na Vivez wadaiwa kuiba kipande cha wimbo wa msanii wa Cuba Livan
Image caption Shakira na Vivez wadaiwa kuiba kipande cha wimbo wa msanii wa Cuba Livan

Mwanamuziki kutoka Cuba amewasilisha malalamishi dhidi ya nyota wa muziki wa Pop Shakira na Carlos Vivez akiwatuhumu kuchukua kipande kidogo cha wimbo wake alioandika miaka kumji iliopita.

Wimbo uliopata ummarufu mkubwa Bicicleta ulioimbwa na na Shakira na Vives ulishinda tuzo za Gramyy miongoni mwa mataifa ya Latino mwaka uliopita.

Msanii huyo wa Cuba, Livan anadai kwamba Shakira na Vivez walinakili mshororo na kipande kidogo cha kibwagizo cha wimbo wake wa 1997 Yo Te Quiero Tanto {I Love You So much} iliochapishwa na kampuni ya muziki ya Sony.

Mahakama ya Uhispania ambapo Shakira anaishi itachunguza madai hayo.

Kitengo cha habari cha AFP kinasema kuwa kundi la Shakira limekataa kuzungumza kuhusu kesi hiyo.