Kifo cha Kim Jong Nam: Malaysia yalaani utumizi wa kemikali

Kim Jong nam nduguye wa kambo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kim Jong nam nduguye wa kambo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un

Malaysia imelaani utumizi wa silaha ya kemikali iliyotumika kumuua Kin Jong Nam ambae ni kaka wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini katika uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur mwezi uliopita.

Malaysia hata hivyo haijahusisha Korea Kaskazini na mauaji hayo lakini taarifa ya wizara ya mambo ya nje imeelezea wasi wasi wake kutokana na utumiaji wa kemikali hiyo ambayo ilihatarisha maisha ya raia wengi.

Taarifa hio imejiri saa chacha baada ya Korea Kaskazini kupinga matokeo ya upasuaji wa maiti uliofanywa na maafisa wa Malaysia na kupata kwamba Kemikali ya VX ilitumika kumuua Kim Jong Nam.