Utafiti: Binaadamu walichangia upanzi wa miti ya Amazon

Binaadamu walichangia kaika upanzi wa miti ya Amazon kulingana na Utafiti
Image caption Binaadamu walichangia kaika upanzi wa miti ya Amazon kulingana na Utafiti

Utafiti mpya umebaini kwamba jamii za jadi katika maeneo ya Amazon zilichangia pakubwa katika upanzi wa miti iliyounda misitu ya sasa asilia.

Hii ni kinyume na ilivyodhaniwa kwamba jamii hizo za jadi hazikuchangia kuwepo misitu hiyo.

Utafiti unasema jamii hizo zilitumia vyakula kama vile njugu karanga, kakao na mafuta yanayopatikana kwenye misitu hiyo.

Utafiti unasema kwamba jamii hizo ziliishi ndani ya misitu hiyo na siyo pembezoni kama ilivyokua imani ya hapo awali.