Zimbabwe yaomba fedha kukabiliana na mafuriko

Serikali ya Zimbabwe imetaka msaada kukabiliana na mafuriko nchini humo
Image caption Mafuriko nchini Benin.

Baada ya kushuhudia msimu wa kiangazi, Zimbabwe sasa imeomba msaada wa dola milioni laki moja kusaidia athari za mafuriko.

Mamlaka zinasema karibu watu 250 wamekufa maji tangu taifa hilo kushuhudia mvua za ghafla, kusini na kusini magharibi mwa nchi.

Serikali imeongezea kwamba mafuriko ya sasa yameharibu vijiji, barabara, mimea na mifugo.

Wiki jana utawala huo unaokumbwa na uhaba wa fedha ulikosolewa kwa kufadhili karamu ya kifahari kusherehekea siku ya kuzaliwa kwa Rais Robert Mugabe iliyogharimu mamilioni ya dola.