Inamaanisha nini kuwa msanii wa kike Afrika?
Huwezi kusikiliza tena

Wanamuziki wa kike wananyanyaswa na kubaguliwa.

Wanawake ulimwenguni wanaadhimisha siku ya uhuru wa muziki hivi leo. Pia ni siku ya kusherehekea wanamuziki waliopigwa marufuku na kufungwa jela kutokana na sanaa yao. Jijini Nairobi maadhimisho ya leo yameandaliwa na shirika la 'Turning Tables Kenya'. Anthony Irungu amezungumza na mwanamuziki wa Kenya Sharon Alai ama MC Sharon, kuhusu maana na umuhimu wa siku ya leo kwa wasanii wa kike.