Wapata mlo na kisha kutimka mbio kutoka hotelini bila kulipa

Watu hao walitimka mbio kutoka mgahawa wa El Carmen Haki miliki ya picha Google
Image caption Watu hao walitimka mbio kutoka mgahawa wa El Carmen

Takriban watu 120 waliokuwa wakipata maankuli kwenye mgahawa mmoja kaskazini magharibi mwa Uhispania, walikimbia wote kwa pamoja na kukosa kulipa.

Watu hao raia wa Romania ambao walikuwa mwanzo wamelipa euro 900, waliondoa kwenye mgahawa wa El Carmen wati walikaribia kupata mlo wa keki.

"Ilitokea kwa dakia moja tu, ni kitu walikuwa wamepanga kwa sababu walitoka kwa kutimka mbio." alisema mmiliki wa hoteli Antonio Rodriguez .

Sasa wana deni la euro 2,000 kwenye hoteli hiyo.

Watu hao walikuwa wamepata chakula cha kwanza, chakula kikuu, na chupa 30 za mvinyo, na Rodriguez anasema kuwa hiyo ndiyo mara ya kwanza ndani ya miaka 35 amefanya kazi ya hoteli kushuhudia kisa kama hicho.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii