China yaongeza bajeti yake ya jeshi

China yaongeza bajeti yake ya kijeshi siku chache baada ya Marekani kutangaza hatua kama hiyo Haki miliki ya picha AP
Image caption China yaongeza bajeti yake ya kijeshi siku chache baada ya Marekani kutangaza hatua kama hiyo

China imesema itaongeza bajeti ya matumizi ya jeshi lake, kwa karibu asilimia saba mwaka huu.

Tangazo hilo limetolewa siku kadhaa baada ya Rais wa Marekani Donald Trump, kutoa muongozo wa mpango wake wa kuongeza bajeti ya matumizi ya jeshi la Marekani, kwa karibu asilimia kumi.

Katika miaka ya hivi karibuni, China imekuwa katika harakati ya kuboresha vikosi vyake vya uslama kadri uchumi wake unavyoendelea kukuwa lakini bajeti yake ya ulinzi bado ni ndogo ikilinganishwa na ile ya Marekani.