Asema alilazimishwa kukiri kumuua Kim Jong nam na Malaysia

Ri Jong Chol asema alihujumiwa na Malayasia
Image caption Ri Jong Chol asema alihujumiwa na Malayasia

Mtu mmoja anayeshukiwa kuhusika na mauji ya ndugu wa kambo wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amesema kuwa yeye ni mhanga wa hujuma za utawala wa Malaysia dhidi ya Korea Kaskazini.

Akizungumza mjini Beijing baada ya kuwasili kutoka Malaysia, Ri Jong Chol, amelaumu polisi wa Malaysia, kwa kutishia familia yake, iwapo hatakiri kuhusika kwake na mauaji ya Kim Jong Nam.

Hapo jana Ijumaa maafisa nchini Malaysia walisema, wana ushahidi wa kutosha, kumfungulia mashtaka Bw. Ri, na kwamba atarejeshwa kwao kwa kosa la kukiuka sheria ya uhamiaji ya nchi hiyo.