Mourinho awataka Wayne Rooney na Ibrahimovic kusalia United

Jose Mourinho awataka Wayne Ibrahimovic na Wayne Rooney kusalia Man United Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Jose Mourinho awataka Wayne Ibrahimovic na Wayne Rooney kusalia Man United

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anasema kuwa anataka Wayne Rooney kusalia katika klabu hiyo asilimia 100 huku akiomba kwamba Zlatan Ibrahimovi pia naye ataongeza kandarasi yake na klabu hiyo.

Rooney mwenye umri wa miaka 31 alitangaza wiki iliopita kwamba atasalia Old Trafford baada ya kuhusishwa na uhamisho wa China.

Nahodha huyo wa timu ya Uingereza pia amehusishwa na uhamisho wa kurudi Everton alikotoka kabla ya kujiunga na Man United, lakini Mourinho anasema kuwa mazungumzo kuhusu uhamisho huo hayana msingi.

Kandarasi ya mshambuliaji Ibrahimovic ya mwaka mmoja pia inamruhusu kuongeza kandarasi ya mwaka mwengine.

Image caption Ibrahimovic na Wyane Rooney

Raia huyo wa Sweden mwenyen umri wa miaka 35 amefunga mabao 26 katika mechi 38 alizochezea United tangu alipojiunga na klabu hiyo kutoka PSG mnamo mwezi Julai.

Alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-2 wa fainali ya kombe la EFL dhidi ya Southampton siku ya Jumapili.

Baada ya fainali, Ibrahimovic alisema kuwa ataamua la kufanya kuhusu hatua ya kuongeza kandarasi yake.