Vyuo vikuu Guinea vyapatikana na wanafunzi 47,000 bandia

Vyuo vikuu Guinea vyapatikana na wanafunzi 47,000 bandia
Image caption Vyuo vikuu Guinea vyapatikana na wanafunzi 47,000 bandia

Mamlaka nchini Guinea imesema kuwa kuna zaidi ya wanafunzi bandia 47,000 katika vyuo vikuu vya taifa hilo.

Takwimu hizo zilichapishwa siku ya Alhamisi na waziri wa elimu ya juu baada ya usajili wa kielektroniki.

Mpango huo uliwafutilia mbali wanafunzi hewa.

Mamlaka ya Guinea hutoa ruzuku kwa vyuo vikuu kulingana na idadi ya wanafunzi.

Waandishi wa habari wanasema vyuo vikuu vya umma vimejaa na ruzuku hizo hutolewa kushinikiza upanuzi katika vyuo vikuu vya kibinafsi.

Hatahivyo baadhi ya vyuo vya kibinafsi vimeongeza idadi bandia ya wanafunzi ili kupata ruzuku zaidi.

Hakuna tamko lolote la vile serikali itakavyokabiliana na madai hatua hiyo