Korea Kusini imewaongezea fedha wale wanaokimbia Korea Kaskazini hadi dola 860,000

Mpaka kati ya Korea Kaskazini na Kusini ni moja ya maeneo yenye ulinzi wa juu zaidi duniani Haki miliki ya picha AP
Image caption Mpaka kati ya Korea Kaskazini na Kusini ni moja ya maeneo yenye ulinzi wa juu zaidi duniani

Korea kusini imeidhinisha nyongeza ya fedha inazotoa kama malipo kwa watu wanaoasi uraia wao kutoka nchi jirani ya Korea Kaskazini,kwa lengo la kupata habari muhimu za kujasusi.

Hatua hiyo pia ina walenga wanajeshi wanaovuka mpaka wakiwa na zana za kijeshi.

Waasi waliyo na taarifa muhimu itakayo saidia kuimarisha usalama wa Korea Kusini, watapokea,fedha ya hadi dola 860,000

Wizara ya masuala ya muungano imesema, sheria hiyo mpya, itaongeza ruzuku ya vifaa vitakavyo ingizwa nchini humo na waasi hao.

Vifaa hivyo ni kama vile meli na karakana ya kijeshi.

Hii ni mara ya kwanza kwa nyongeza kama hiyo kutolewa katika kipindi cha miaka ishirini.

Lengo la hatua hiyo ni wazi kuwa, Korea Kusini inataka kuongeza idadi ya watu wanaobadilisha uraia wa Korea kaskazini kujiunga nayo.

Serikali ya Korea Kaskazini bado haijatoa tamko lolote juu ya hatua hiyo ya Korea Kusini.