Mexico yafungua vituo miji 50 nchini Marekani kutetea raia wake

Wahamiaji wanaohusishwa na makosa madogo ya kuvunja sheria za barabara wanaweza kutimuliwa Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Wahamiaji wanaohusishwa na makosa madogo ya kuvunja sheria za barabara wanaweza kutimuliwa

Mexico imefungua vituo vya kutoa msaada wa kisheria katika balozi zake katika miji 50 ya Marekani, ili kulinda raia wake kutokana na utekelezaji mkali wa sheria za uhamiaji nchini humo.

Wakati wa ziara ya maafisa wakuu wa Marekani nchini Mexico mwezi uliyopita, utawala wa nchi hiyo ulielezea wasiwasi wake juu ya sera ya Trump ya uhamiaji dhidi ya raia wake.

Inakadiriwa kuwa takriban raia milioni sita wa Mexico wanaishi nchini Marekani kinyume cha sheria.

Vituo hivyo vipya vitatoa msaada wa sheriak wa raia wa Mexico ambao wanahisi kuwa haki zao ziko hatarini nchini Marekani.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maandamano ya kupinga watu kufukuzwa yamesababisha watu kukamatwa kote Marekani

Uhusiano kati ya Mexico na Marekani umekuwa mbaya zaidi tangu miango kadha iliyopita.

Wiki moja baada ya kuapishwa mwezi Januari , Rais Donald Trump alisema kuwa atajenga ukuta kati ya mpaka wa Mexico na Marekani.

Alisisitiza kuwa Mexico italipia gharama ya ujenzi wa ukuta huo.

Matamshi hayo yalisababisha rais wa Mexico Enrique Pena Nieto, kufuta safari yake nchini Marekania tarehe 31 mwezi Januari. na kutangaza ufadhili zaidi kulinda haki za za raia wa Mexico walio nchini Marekani.

Image caption Mpaka kati ya Marekani na Mexico