Rubani wa ndege ya jeshi la Syria iliyoanguka apatikana

Ndege hiyo ilitajwa kuwa aina ya MiG-23 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndege hiyo ilitajwa kuwa aina ya MiG-23

Rubani wa ndege ya jeshi la Syria, ambayo ilianguka karibu na mpaka kati ya Syria na Uturuki amepatikana akiwa hai na kupelekwa hospitalini.

Rubani huyo ambaye alirukoa kutoka kwa ndege hiyo ametambuliwa kuwa raia wa Syria.

Haijulikani ni kipi kilisababisha ndege hiyo ianguke kusini mwa Uturuki.

Kundi la wanamgambo ambalo linapigana na rais wa Syria Bashar al-Assad lilisema kuwa ndege hiyo ilidunguliwa lakini serikalia ya Syia haijatamka lolote.

Mapema jeshi la Syria lilisema kuwa lilikuwa limepoteza mawasiliano na ndege yake karibu na mpaka.

Rubani huyo alipatikana akiwa amechoka baada ya shughuli ya kumtafuta iliyodumu saa tisa.

Alipelekwa hospitalini katika wilaya ya Hatay, lakini hakuna taarifa zilizotolewa kuhusu hali yake.

Image caption Hatay nchini Syria