Mwili wa mjerumani aliyekatwa kichwa Ufilipino wapatikana

Jurgen Kantner na mkewe Sabine Merz wote waliuawa Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jurgen Kantner na mkewe Sabine Merz wote waliuawa (picha maktaba)

Mwili wa raia wa Ujerumani ambaye alikatwa kichwa na wanamgambo wa kiislamu nchini Ufilipino wiki hii umepatikana.

Jurgen Kantner aliyetekwa nyara kutoka kwa mashua yake ya kifahari mwezi Novemba. Kundi la wanamgambo wa Abu Sayyaf linasema kuwa ndilo lilihusika.

Mwili huo ulipatikana katika kisiwa cha Sulu na utarudishwa nchini Ujerumani.

Mwili wa mkewe Kantner, Sabine Merz ulipatikana ukiwa na jeraha la risasi ndani ya mashua hiyo iliyokuwa imetelekezwa mwezi Novemba

Mwezi uliopita video ilichapishwa ikionyesha mjerumani huyo akikatwa kichwa, muda mfupi baada ya muda uliokuwa umetangazwa wa kulipwa fidia kukamilika.

Wizara ya mambo ya nchi za kigeni ya Ujerumani ilisema kuwa imepata mshutuko mkubwa kufuatia kitendo hicho cha kinyama.

Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte mapema alikuwa ameoomba msamaha Ujerumani na familia ya Kantner, kwa kushidwa kumuokoa kwa karibu miezi minne lakini akasisitiza kuwa fidia haitalipwa.

Abu Sayyaf ni moja ya makundi madogo zaidi lenye ghasia mbaya kusini mwa Ufilipino, kutokana na dhuluma zake ikiwemo ukataji vichwa.

Kundi hilo limetangaza kulitii kundi la Islamic State.

Haki miliki ya picha Abu Sayyaf
Image caption Abu Sayyaf limetangaza kulitii kundi la Islamic State.