Fillon ajipigania kwa kutoa hotuba kali Paris

Umati uliohudhuria mkutano wa Fillon Haki miliki ya picha AFP
Image caption Umati uliohudhuria mkutano wa Fillon

Wafuasi wa mwanasiasa wa sera zisizopendelea mabadiliko, Francois Fillon, wamekusanyika kwa mkutano wa hadhara mjini Paris, katika jaribio la mawisho, kuonyesha kuwa uchunguzi kuhusu uhalifu, anaokabili, hautomzuwia kushinda katika uchaguzi wa rais.

Fillon amewashauri wafuasi wake kuwa wakakamavu wakati akihutubia umati mjini Paris.

Aliuambia umati huo wa maelfu ya watu kuwa ataondolewal madai kuwa allimlipa mkewe na watoto kwa kazi ambayo hawakuifanya

Haki miliki ya picha AP
Image caption Francois Fillon

Mkutano huo unaonekana kama mtihani kwa umaarugu wa Bwaan Fillon.

Kura za maoni zinaonyesha, kuwa asilimia 70 ya wapigaji kura, wanataka atoke katika mashindano.

Viongozi wa chama chake watakutana kesho, kuamua hatima yake.

Mwandishi wa BBC mjini Paris, anasema Bwana Fillon atahitaji watu angalau elfu 50 kuhudhuria, lakini wale wanaomlaumu, wanasema kuwaleta wafuasi kwa mabasi kutoka eneo lake la Kikatoliki, haitosaidia.

Bwana Fillon amekanusa mara kadha, kwamba aliwalipa mishahara mkewe na watoto, kwa kazi ambayo hawakufanya.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Penelope Fillon amemshauri mumewe kuendelea hadi mwisho