Fillon:siondoki kwa shinikizo

Fillon Haki miliki ya picha AFP
Image caption Francois Fillon amekuwa akipata mashinikizo kutowania nafasi ya urais nchini Ufaransa

Mgombea wa Chama cha Republican nchini Ufaransa, Francois Fillon ambaye anafanyiwa uchunguzi kuhusu malipo aliyoyafanya kwa familia yake amesema hakuna wa kumshinikiza kubadili nia ya kugombea nafasi ya urais.

Katika mahojiano kwa njia ya Televisheni amesisitiza kuwa kampeni zake zitaendelea ingawa amekuwa akipata upinzani kutoka kwa baadhi ya wanachama wa Republican.

Viongozi wa chama watakutana siku ya Jumatatu kuamua cha kufanya huku baadhi wakitaka aliyekuwa waziri mkuu wa Ufaransa Alan Juppe' kuchukua nafasi ya Fillon.

Bwana Juppe amesema atatoa tamko siku ya Jumatatu.

Baadhi ya watu wanaomuunga mkono bwana Fillon wametishia kura zao kuzipeleka kwa mgombea wa chama cha National Front iwapo watamshinikiza kuondoka.