Waasi washambulia kambi ya jeshi Mali

Waasi wa Tuareg nchini Mali wadaiwa kukishambulia kituo kimoja cha jeshi
Image caption Waasi wa Tuareg nchini Mali wadaiwa kukishambulia kituo kimoja cha jeshi

Waasi wenye silaha nchini Mali wameshambulia kambi ya jeshi karibu na mpaka wa Burkina Farso ambako wanajeshi 11 walifariki.

Kuna makundi kadhaa ya wapiganaji yanayoendesha shughuli zake katika eneo hilo na haijulikani ni nani hasa alifanya mashambulizi hayo.

Shahidi mmoja alisema alishuhudia wapiganaji hao wakipora silaha nyingi za kijeshi katika eneo hilo.

Wakati huohuo kuna ripoti kuwa jiji la Timbuktu limezingirwa na makundi yenye silaha yanayopinga Serikali.

Inadaiwa kuwa makundi hayo yameziba njia za kuingia na kuondoka katika jiji hilo.