Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia bado hajaondoka nchini Malaysia hata baada ya kupewa saa 48 kuondoka

Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia bado hajaondoka nchini Malaysia hata baada ya kupewa saa 48 kuondoka
Image caption Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia bado hajaondoka nchini Malaysia hata baada ya kupewa saa 48 kuondoka

Balozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia anakabiliwa na notisi ya kuondoka nchini humo kufuatia mgogoro kuhusiana na uchunguzi wa kifo cha Kim Jong nam nduguye wa kambo rais wa Korea kaskazini.

Siku ya Jumamosi balozi Kang Chol alipewa ilani ya saa 48 kuondoka nchini humo.

Mamlaka ya Malaysia imeishtumu Pyongyang kwa kujaribu kuingilia uchunguzi huo.

Korea Kaskazini nayo imekataa ripoti ya upasuaji ambayo inaonyesha kuwa King Jong nam alifariki baada ya wanawake wawili kumpaka sumu aina ya VX aktika uso wake.