Tristan Voorspuy alikuwa anamiliki shamba kubwa nchini Kenya

Aalihudumu katika jeshi la Uingereza kwa miaka sita Haki miliki ya picha OFFBEAT SAFARIS
Image caption Tristan Voorspuy ni raia wa Uingereza mwenye shamba kubwa huko Laikipia aliyeuawa kwa kupigwa risasi

Juhudi za kuutafuta mwili wa raia wa Uingereza anayemiliki shamba kubwa ambaye alipigwa risasi na wafugaji waliojihami nchini Kenya wikendi iliopita mjini Laikipia zimefeli baada ya watu waliokuwa wamejihami kulifyatulia risasi kundi la wasakaji waliotumwa na familia yake kulingana na gazeti la the Star nchini Kenya.

Tristan Voorspuy aliuawa na wafugaji wakati alipoenda kuchunguza baadhi ya nyumba zake ambazo zilikuwa zimechomwa na washambuliaji hao.

Laikipia na kaunti jirani zimekuwa zikikabiliwa na viwango vya juu vya ghasia zinazosababishwa na wafugaji ambao wanatafuta lishe ya mifugo yao lakini, wachanganuzi wanasema kuwa utovu huo wa usalama umesababishwa na siasa.

Wamiliki wa mashamba makubwa mjini Laikipia wameitaka serikali kueka usalama katika eneo hilo.

Wanahofia kwamba tatizo hilo huenda likaenea katika kipindi cha wiki zijazo huku ardhi ya lishe ikipungua katika maeneo ya wafugaji hao kutokana na ukame katika maeneo ya kaskazini mwa taifa hilo.

Wakati huohuo kuna hali ya wasiwasi katika kaunti jirani ya Baringo baada ya serikali kupeleka mamia wa maafisa wa usalama na kutoa agizo la kupiga risasi wafugaji wanaofanya mashambulio.