Mwalimu anayewafunza wanamuziki wengi Tanzania
Huwezi kusikiliza tena

Mwalimu anayewafunza wanamuziki wengi Tanzania

Nchini Tanzania ili kuumudu muziki kibiashara, wanamuziki wengi vijana hulazimika kupita mikononi mwa kijana kutoka nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwa jina Ticha au Kanali Jento.Ni Misheli Omba Otenga Kyoso msomi wa ngazi ya Chuo Kikuu mtaalamu wa Forodha.

Kutokana na kipaji chake cha muziki alihamia Afrika ya Kusini lakini muziki wa kule haukumwendea vizuri hadi alipohamia Zambia ambako alianza kufanya kazi na Mwanamuziki Suke Chile. Kanali Jento alihamia Tanzania mwaka 1994 na kujiunga na Beta Muzika kabla ya kuanzisha The Dream Team FM Academa na baadaye akishirikiana na Mkongo mwenzake aliyefahamika kwa jina Ndanda Kosovo wakaanzisha Stono Muzika 'wajelajela. Kwa kipindi cha miaka alielekea Muscat kwa kazi za muziki kabla ya mwaka 2005 kurejea Tanzania na kuanza kufundisha muziki.

Kwa miaka mingi muziki wa Tanzania ulipoteza ladha yake ya awali kwa kukosa kuimba moja kwa moja na bendi huku ala za muziki zikipigwa jukwaani kwani vijana wa kizazi kipya walianza kutumia sauti zilizorekodiwa studioni. Wale waliogundua hali hiyo inadidimiza muziki wakatamani kujifunza kuimba pasina kutegemea studio, ndipo Kanali Jento akaanza kuwafundisha muziki wa ala na uimbaji.

Unaweza kuyasikiliza hapa mazungumzo kati ya Misheli Omba Otenga Kyoso 'Kanali Jento' na mwandishi wa BBC Arnold Kayanda.