Matatizo ya usingizi yaongezeka miongoni mwa watoto mara kumi

Ellie Keady
Image caption Ellie Keady hulala saa tatu za usiku, lakini kwa kawaida huwa macho hadi saa nane na nusu usiku

Idadi ya wahudumu wa hospitali wanaowahudumia watoto wa chini ya miaka 14 nchini Uingereza wanaoshughulikia matatizo ya usingizi imeongezeka mara tatu katika kipindi cha miaka 10, kwa mujibu wa data zilizochunguzwa na kitengo cha BBC Panorama.

Dawa zinazotolewa kwa ajili ya usingizi wa kawaida aina ya melatoni zimeongezeka mara kumi zaidi kwa watoto na watu wazima wenye chini ya umri wa miaka 55 katika kipindi hicho hicho.

Ukosefu wa usingizi wa kutosha miongoni mwa watoto umehusishwa na uzito unene wa kupindukia, kiwango cha chini cha kinga ya mwili, na matatizo ya afya ya akili.

Pia umehusishwa na kushindwa kudhibiti hisia na matokeo mabaya ya masomo ya shule.

Nini huchangia ukosefu wa Usingizi?

Masuala mbali mbali juu ya maisha tunayoishi sasa yanadhaniwa kuchangia kuvuruga usingizi wa watoto:

Mwangaza wa blu unaotolewa na simu za smartphones na tablets unafahamika kwa kupunguza kiwango cha uzalishaji vichocheo asilia vya melatonin, ambavyo hutufanya tusinzie.

Image caption Dr Hill anaonya kuwa matatizo ya usingizi yameongeza gharama kubwa katika hospitali ya watoto ya Southampton

Wazazi wawili wanaofanya kazi wanaoishi katika nyumba moja na kuendelea kufanya kazi jioni wawapo nyumbani husababisha muda wa kulala kusogezwa mbele zaidi.

Hali kadhalika vinywaji baridi vyenye gesi, viwango vya juu vya sukari na Caffeine pia huwafanya watoto kukosa usingizi usiku.

Ellie Keady, mwenye umri wa miaka 13, hivi karibuni alikuwa chini ya uangalizi wa hospitali ya watoto ya Sheffield inayochunguza matatizo ya usingizi wakati wa usiku iliyoshuhudia kuongezeka mara kumi kwa idadi ya watoto wenye matatizo ya usingizi.

Ellie hulala saa tatu za usiku, lakini kwa kawaida huwa macho hadi saa nane na nusu usiku

"mara nyingine huwa ninaenda shule baada ya kulala saa mbili na nusu pekee ,"alisema.

Ukosefu wa usingizi umeathiri elimu yake.

Mahudhurio yake ya shule yamekuwa mabaya kutokana na kuugua kutokana na uchovu na maambukizi ya virusi vitokanavyo na upungufu wa kinga ya mwili.

"Iwapo utapiga chafya katika chumba chake , Ellie atapata mafua," anasema mama yake, Joanne.

Ellie alianza kuwa na maatizo ya usingizi tangu mwaka 2011 alipovunjika mguu. Hakuweza kutembea kwa miezi kadhaa na uzito wake wa mwili ulianza kuongezeka.

Hivi karibuni alipoteza kila 16 katika kipindi cha miezi sita baada ya kupunguza kiwango cha mlo na kufanya mazoezi, lakini kupunguza mlo imekuwa changamoto kwake.

Watafiti wanasema kuna uhusiano wa kuaminika baina ya ukosefu wa usingizi na kuongezeka kwa uzito wa mwili miongoni mwa vijana wadogo.

Viwango vya chini vya usingizi vinadhaniwa kuvuruga uwiano wa vichocheo vya mwili/homoni vinavyoufahamisha ubongo wetu kuwa tumeshiba ama tuna njaa, na hivyo inakuwa vigumu kudhibiti hamu ya chakula.

Tunapochoka, tunakuwa na uwezekano mkubwa wa kuwa na hamu kubwa ya chakula chenye viwango vya juu vya sukari na mafuta.