Kashfa za udukuzi wa Urusi zinavyoendelea kumzonga Trump

Donald Trump na Vradimir Putin Haki miliki ya picha AFP/GETTY
Image caption Uswahiba wa Donald Trump na rais wa Urusi Vradimir Putin umezingirwa na shuku

Katika kipindi chote cha mkanganyiko wa kampeni za Donald Trump na matukio ya ghasia yaliyogubika siku zake za mwanzo ndani ya Ikulu ya White , kuna utata mmoja uliokwama kama gundi dhidi ya utawala wa Trump, nao unaihusu Urusi.

Kuondoka mamlakani ghafla kwa Michael Flynn kama mshauri wa usalama wa taifa mwezi wa Februari na pia kufichuliwa kwa mikutano baina ya Mwanasheria Mkuu Generali Jeff Sessions na balozi wa Urusi Sergei Kislyak kumekuwa moja ya mambo yenye utata Marekani unaotishia maslahi ya Urusi.

Onyo la awali

Ilikuwa mwezi Mei 2016 ambapo ripoti ya kwanza iliibuka juu ya wadukuzi waliolenga chama cha Demokratic. Katika kipindi cha miezi miwili iliyofuata, taarifa zilieleza kuwa mashirika ya ujasusi ya marekani yalibaini uingiliaji wa taarifa uliofanywa na wadukuzi wa Urusi.

Mwezi Julai, Katika siku ya Mkutano mkuu wa Kitaifa wa chama cha Democratic , mtandao wa Wikileaks ulichapisha ujumbe wa maandishi 20,000 wa ndani ulioibiwa na wadukuzi.

Maafisa wa ujasusi wa Marekani walisema kuwa wanaamini "kwa kiwango cha juu" kwamba Urusi ilihusika katika udukuzi huo, lakini maafisa wa kampeni wa Trump walikataa wazi matokeo ya uchunguzi huo wa kijasusi.

Badala yake katika mkutano na waandishi wa habari, Bwana Trump alichochea hisia kali kwa kuwakaribisha wadukuzi wa Urusi kulenga hifadhi ya barua pepe binafsi zenye tata za Bi Hillary Clinton, akisema : "Urusi, kama unasikia, natumai una uwezo wa kutafuta, ujumbe wa barua pepe 30,000 ambazo zimepotea".

Haki miliki ya picha AP
Image caption Michael Flynn akishiriki meza moja ya chakula na kiongozi wa Urusi Vladimir Putin mnamo mwezi Disemba, 2015

Katika kipindi hicho sakata ya kashfa ya udukuzi ilianza kujitokeza, Meneja wa kampeni ya Bwana Trump wakati huo , Paul Manafort, alishutumiwa kwa kukubali mamilioni ya dola pesa taslimkwa ajili ya kuwakilisha maslahi ya Urusi ndani ya Ukraine na Marekani, ikiwemo kuwasiliana na wafanya biashara wakuu wenye ushawishi mkubwa wenye uhusiano wa karibu na waziri mkuu wa Urusi Vladimir Putin.

Huku Bwana Manafort akiongoza kampeni, Chama cha Republican kilibadilisha lugha katika sera yake kuhusu mzozo nchini Ukraine , kuachana na hisia za chuki dhidi ya Urusi, zilizodaiwa kuwa miongoni mwa wawakilishi wawili wa kampeni za Trump.

Bwana Manafort alichunguzwa na FBI na kujiuzulu kama mwenyekiti wa kampeni ya Bwana Trump. Sawa na Bwana Flynn, Bwana Manafort, mwanasiasa mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 40, alitakiwa kuzima baadhi ya ya ghasia na utata unaomzingira Bwana Trump, lakini aliishia kujipata matatizoni.

Mwezi Oktoba, taasisi za ujasusi za Marekani zilitoa kauli ya pamoja rasmi ikiishutumu Urusi kwa kuhusika na udukuzi wa taarifa za Kamati ya Taifa ya chama cha Democratic (DNC).

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Michael Flynn alihamasisha kulainishwa kwa sera ya Marekani kwa Urusi

Bwana Trump aliendelea kupinga matokeo ya taasisi hizo,akidai katika mdahalo kuhusu uchaguzi wa urais kwamba "inaweza kuwa Urusi, lakini pia inaweza kuwa pia kuwa ulifanywa na Uchina, wanaweza pia kuwa watu wengine wengi. Anaweza pia kuwa mtu fulani mwenye uzito wa paund 400 aliyeketi kwenye kitanda chake".

Katika siku hiyo hiyo mashirika ya ujasusi yalitoa ripoti ya uchunguzi wake, iliyoiywa "udukuzi wa Hollywood" ambapo zilipatikana kauli zilizorekodiwa za matusi ya aibu alizozitoa Bwana Trump juu ya wanawake mwaka 2005. Sa moja baadae, mtandao wa Wikileaks ukaanza kutuma maelfu zaidi ya barua pepe za Bi Clinton. Bwana Trump aliendelea kukataa kukubali kwamba Urusi ilihusika katika udukuzi huo.

Ushahidi dhidi ya Flynn...

Mnamo mwezi Februari sakata lililokuwa kubwa dhidi ya Urusi hatimae likalipuka , miezi kadhaa miongoni mwa maafisa wa ujasusi.

Ripoti ya gazeti la Washington Post lilisema kuwa Bwana Flynn alijadili uwezekano wa Bwana Obama wa kuondoa vikwazo vyake dhidi ya Urusi pamoja na balozi wa Urusi , Sergei Kislyak, kabla ya Bwana Trump kuingia mamlakani.

Bwana Flynn,ambaye alionekana mara kwa mara katika kituo cha televisheni cha propaganda za Urusi RT wakati mmoja alishiriki meza moja ya chakula na Bwana Putinkama mshauri wa usalama wa taifa wa Bwana Trump.

Ni marufuku kisheria kwa raia wa kawaida wa Mrekani kufanya mazungumzo ya kidiplomasia ya Marekani.