Jeshi la Uingereza lilikatazwa kuokoa wasichana wa Chibok

Wasichana wa Chibok waliotekwa nyara mwaka 2014 Haki miliki ya picha AFP
Image caption Wasichana wa Chibok waliotekwa nyara mwaka 2014

Vikosi vya jeshi la Uingereza vilitoa pendekezo la kufanya jaribio la kuwakoa karibu wasichana 300, waliotekwa nyara na wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram, lakini pendekezo lao likakataliwa na aliyekuwa rais wa Nigeria wakati huo Goodluck Jonathan.

Kwenye oparesheni iliyopewa jina, Operation Turus, jeshi la Uingerezea lilifanya uchunguzi katika anga ya Nigeria kwa miezi kadha baada ya kutekwa kwa wasichana hao kutoka shule ya Chibok mwaka 2014, , kwa mujibu wa gazeti la the Observer.

"Eneo wasichana hao walikuwa lilitambuliwa wiki chache za kwanza , tulipendekeza kuwaoko lakini serikali ya Nigeria ikakataa, waliohusika kwenye oparesheni hiyo waliliambia gazeti la the Observer.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Goodluck Jonathan

Hata hivyo aliyekuwa rais wa Nigeria Goodluck Jonathan amekana ripoti kuwa alikataa pandekezo kutoka kwa jeshi la Uingereza la kuokolewa kwa wasichana hao.

Msemaji wa Jonathan Ikechukwu Eze, alisema kuwa ushirikiano wa kimataifa kuwaokoa wasichana hao ulizihusisha nchi majirani na utawala wa Jonathan uliunga mkono jitihada hizo na pia kuruhusu wanajeshi wa nchi za magharibu kufanya uchunguzi katika anga ya nchi hiyo.

Msemaji wa serikali ya sasa aliiambia BBC kuwa ripoti ya the Observer, ilithibitisha kuwa bwana Jonathan alikuwa akilitumia kisiasa suala la Boko Haram.