Mzozo wa dhahabu wasababisha watu 4 wa familia moja kuuawa Ufaransa

Familia ya Troadec ilionekana mara ya mwisho tarehe 16 mwezi Februari mwaka huu Haki miliki ya picha AFP
Image caption Familia ya Troadec ilionekana mara ya mwisho tarehe 16 mwezi Februari mwaka huu

Ndugu wa watu wanne wa familia moja ambao wamekuwa hawajulikani waliko nchini Ufaransa tangu kati kati ya mwezi Februari amekiri kuwa ndiye aliwaua.

Aliyekuwa shemeji wa familia ya Pascal Troadec kwa jina Hubert C, anaripotiwa kuwaambia wachunguzi kuwa aliwaua kutokana na mzozo wa umiliki wa dhahabu.

Inaamiwa kuwa aliwaua kwa kuwapiga kwa kifaa butu nyumbani kwao eneo la Nantes , kwa mujibu wa gazeti la Le Parisien.

Chembechembe zake za DNA zinaripotiwa kupatikana kwenye nyumba ya watu hao.

Haki miliki ya picha AFP/Getty
Image caption Dadake Pascal Troadec na shemeji wake wa zamani wanahojiwa Brest

Alikamatwa pamoja dadake Troadec, ambaye ni mke wawe wa zamani eneo la Brest, na vyombo vya habari vinasema kuwa bidhaa za familia hiyo vilipatikana eneo hilo.

Pascla na Brigitte wote wenye umri wa miaka 49, mtot wao wa kiume Sebastien 21, na binti yao Charlotte 18, walionekana mara ya mwisho Februari tarehe 16.

Haijaripotiwa ikiwa Hubert C, amewaambia polisi ilipo miili yao.

Mzozo huo wa urithi unaripotiwa kuzuka kutokana na dhahabu iliyopatikana wakati wa ukarabati wa nyumba eneo la Brest, iliyomilikiwa na baba yake Troadec ambaye alifariki miaka kadha iliyopita.

Image caption Ramani ya Nantes, Brest na Saint-Nazire nchini Ufaransa
Haki miliki ya picha AFP
Image caption Bidhaa za Charlotte zilipatikana eneo lenye miti