Waliomtoa mtoto wa miaka 10 kafara wakamatwa India

Taarifa hizo zilisambaa na kundi la watu likakusanyika nje nyumba ya watu hao na kuanza kurusha mawe Haki miliki ya picha Karnataka police
Image caption Taarifa hizo zilisambaa na kundi la watu likakusanyika nje nyumba ya watu hao na kuanza kurusha mawe

Polisi kwey jimbo la kusini mwa India la Karnataka wamewakamata watu watatu kwa kuhusika na kumtoa kafara mtoto msichana wa umri wamaia 10.

Polisi waliiambia BBC kuwa mtoto huyo aliuawa kutokana na maagizo ya mchawi ili kumponya mtu aliyekuwa na ulemavu.

Ndugu na dada wa mtu huyo wamekamatwa kwa mashtaka ya kumteka nyara na kumuua msichana huyo.

Inadaiwa kuwa mchawi huyo aliwaambia kuwa hiyo ilikuwa njia pekee ya kutibu uchawi ambao ndugu yaop alikuw aamefanyiwa.

Kijana wa kiume wa umri wa miaka 17 naye amekamatwa kwa kusaidia kumteka nyara mtoto huyo.

Mauaji hayo yaligunduliwa wakati wenye walipata mwili wa msichana huyo ndani ya mfuko. Pia walipata bidhaa ambavyo polisi wanaamini kuwa vilitumiwa kufanyia uchawi.

Taarifa hizo zilisambaa na kundi la watu likakusanyika nje nyumba ya watu hao na kuanza kurusha mawe.

Iliwalazimu polisi kutumia nguvu kuwatawanya watu hao.