Raia wa Nigeria wazuiwa kuingia Marekani

Raia wa Nigeria wazuiwa kuingia Marekani Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Raia wa Nigeria wazuiwa kuingia Marekani

Nigeria imewashauri raia wake wasisafiri kuenda nchini Marekai baada ya watu kadha raia wa nchi hiyo wenye visa halali kuzuiwa kuingia Marekani.

Taarifa hiyo ilitolewa naAbike Dabiri-Erewa, amabaye ni mshauri maalum wa rais kuhusu masuala ya nchi za kigeni.

"Wiki chache zilizopita, ofisi imepokea taarifa chache za raia wa Nigeria waliao na vibali halali vya kuingia Marekani, wanaozuiwa kuingia na badala yake kurejeshwa Nigeria," alisema Bi Dabiri-Erewa.

Anasema hakuna sababu zilizotolewa kwa uamuzi huo unaochukuliwa na maafisa wa uhamiaji wa Marekani.

Aliwashauri wale walio na mpango wa kusafiri kuenda Marekani bila sababu muhimu kubadilisha mpango wao hadi sera mpya za uhamiaji zitakapo bainika.