Trump atia sahihi amri mpya ya kuzuia wahamiaji

Trump atia sahihi amri mpya ya kuzuia wahamiaji Haki miliki ya picha BBC Sport
Image caption Trump atia sahihi amri mpya ya kuzuia wahamiaji

Rais wa Marekani Donald Trump ametia sahihi amri mpya kuu ya uhamiaji ambayo itawazuia wahamiaji kutoka nchi sita zenye waislamu wengi kuingia Marekani kwa muda wa siku 90.

Iraq imeondolewa kutoka kwa orodha ya nchi saba zilizoorodheshwa awali. Watu wenye visa halali wataruhusiwa kuingia Marekani.

Hatua hiyo ambayo pia inajumuisha marufuku ya siku 120 kwa wakimzi wote, itaaza kutekelezwa tarehe 16 Machi.

Amri ya awali ilifutilia mbali mpango mzima wa uhamiaji wa Marekani, na kuwazuia raia kutoka nchi saba zenye waislamu wengi kuingia Marekani.

Hatua hiyo ilizua fujo kwenye viwanja vya ndege wakati watu wenye stakabadhi halali walizuiwa kuingia Marekani na pia kusababisha maandamano makubwa.

Uongozi wa bwana Trump ulisema kuwa amri hiyo ni muhimu kuwalinda Marekani kutokana na ugaidi.

Ilani ya siku 10 imetolewa ili kusaidia kuzuia fujo zilizoshuhudiwa kwenye viwanja vya ndege tarehe 27 mwezi Januari wakati amri ya kwanza ilipotangazwa.

Wasafiri waliokuwa na visa halali waliokua hewani wakati huo walijipata wakizuiwa na maafisa wa mipaka walipowasili.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Rais wa Iraq kama mkalimani wa zamani wa jeshi la Marekani Hameed Darwish, hawatazuiwa tena
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Familia hii ya Wasyria iliungana Chicago mwezi Februari