Korea Kaskazini yasema inajiandaa kushambulia Japan

Image caption Maeneo ambayo makombora yalirushwa

Korea Kaskazini imesema kuwa ulipuaji wa makombora manne hiyo jana ulikuwa mafunzo ya kujiandaa kushambulia vituo vya kijeshi vilivyoko nchini Japan na kwamba shughuli hiyo ilisimamiwa na kiongozi wa Taifa hilo katili Kim Jong-un.

Rais Trump alifanya mashauriano kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Japan, Shinzo Abe, na Rais wa muda wa Korea Kusini kujadili jinsi ya kujibu kitendo hicho.

''Korea kaskazini imefyatua makombora yake manne leo na kuangukia karibu na eneo letu la maji lenye manufaa kwetu kiuchumi.