Israel yawapunguzia hukumu watumizi wa bangi

Shamba la bangi karibu na Safed Kaskazini mwa Israel linaongoza kuhusu utafiti wa utumizi wa bangi kwa matibabu

Chanzo cha picha, AP

Maelezo ya picha,

Shamba la bangi karibu na Safed Kaskazini mwa Israel linaongoza kuhusu utafiti wa utumizi wa bangi kwa matibabu

Serikali ya Israel imechukua hatua ya kupunguza hukumu kwa watumizi wa bangi.

Badale yake imeunga mkono hatua ya kuwapiga faini huku wale wanaorejelea makosa hayo wakishtakiwa kwa uhalifu.

Uuzaji,ununuzi na uzalishaji wa bangi Israel utasalia kuwa kinyume na sheria na mpango huo lazima uidhinishwe na bunge.

Kulingana na afisi ya Umoja wa Mataifa kuhusu uhalifu ,takriban asilimi 9 ya raia wa Israel wanatumia bangi ijapokuwa baadhi ya wataalam wanakadiria kwamba idadi hiyo iko juu zaidi ya inavyodhaniwa.

Hatua hiyo inafuatia mapendekezo ya kamati ilioanzishwa kuangazia swala hilo na imetaja baadhi ya majimbo ya Marekani na Ulaya kwa kuhalalisha utumizi wa dawa hiyo.

''Kwa upande mmoja tunangazia siku zijazo na kwa upande mwengine pia tunaona hatari na hivyobasi tutajaribu kusawazisha maswala hayo mawili'', waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu aliambia bunge kabla ya kura hiyo kupigwa..