Wabunge wa Tanzania na Kenya wavamiwa Afrika Kusini

Wabunge wa Kenya, Tanzania na Msumbiji wavamiwa Johannesburg
Image caption Wabunge wa Kenya, Tanzania na Msumbiji wavamiwa Johannesburg

Wabunge wa bunge la Afrika kutokea mataifa ya Tanzania ,Kenya na Msumbiji walivamiwa na majambazi walipokua wakitoka uwanja wa ndege wa OR Tambo mjini Johannesburg wakielekea hotelini .

Mmoja ya wabunge hao kutokea Kenya alipigwa vibaya na majambazi hao alipokua akijaribu kuzozana nao wasiwaibie .

Wabunge wengi wanasema wakati umefika sasa bunge hilo la Afrika kuhamishwa kutoka Afrika Kusini kwa sababu hakuna usalama wa kutosha nchini humo.