Malasyia na K.Kaskazini zalumbana juu ya kifo cha Kim Jong nam

Kim Jong num
Image caption Malaysia haijailaumu moja kwa moja Korea Kaskazini kwa kifo cha Kim Jong nam, lakini inashuku kwa kiasi kikubwa kwamba serikali ya Pyongyang ilihusika.

Korea Kaskazini pamoja na Malasyia kila moja imezuwia raia wa kutoka nchi nyingine kondoka nchini mwake , katika mzozo unaohusu mauaji ya Kim Jong-nam.

Hatua hizo kali za kulipiza kisasi zinachukuliwa wakati Korea Kaskazini ikigadhabishwa na uchunguzi wa Malasyia unaoendelea kuhusu kifo chake kilichotokea katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kuala Lumpur.

Kaka yake wa kambo rais wa Korea Kaskazini aliuawa kwa sumu ya kemikali inayouwa mishipa ya neva.

Malaysia haijailaumu moja kwa moja Korea Kaskazini kwa kifo hicho, lakini inashukiwa kwa kiasi kikubwa kwamba serikali ya Pyongyang ilihusika na kifo hicho.

Korea Kaskazini imekanusha kwa ukali tuhuma zozote juu ya kuhusika na mauaji hayo na mzozo juu ya nani ana haki ya kudai mwili wa Bwana Kim - umeendelea kuongezeka katika kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Kwa pamoja Malaysia na Korea Kaskazini zimewatimua mabalozi wa mwenzake.

Shirika la habari la serikali ya Korea Kaskazini Tlimesema leo (Jumanne) limesema kwamba "raia wote wa Malaysia kutoka chama cha DPRK (Democratic People's Republic of Korea) watazuwiwa kwa muda kuondoka nchini hadi tukio lililotokea nchini Malasyia litakapotatuliwa ipasavyo". Imesema kuwa hii inalenga kuhakikisha usalama wa raia wake na wanadiplomasia.

Raia wa Malaysian waliopo katika nchi ya Korea Kaskazini wataendelea na maisha yao kama kawaida, liliongeza shirika hilo.

Kwa ghadhabu kubwa waziri mkuu wa Malaysia Najib Razak aliitaja hatua hiyo ya Korea Kaskazini kuwa ya " kuudhi" ambayo ''haikuzingatia sheria zote za kimataifa na taratibu za kibalozi".

Wamalaysia wametekwa nyara nchini Korea Kaskazini, alisema katika kauli yake.

"kuwalinda raia wetu ni jukumu langu la kwanza, na hatutasita kuchukua hatua zote muhimu watakapotishiwa."

Awali, Naibu waziri mkuu Ahmad na waziri wa mambo ya ndani Zahid Hamidi walisema kuwa kwa kujibu hatua ya Korea Kaskazini , wahudumu na maafisa wa ubalozi wa Korea Kaskazini pia hawataruhusiwa kuondoka.

"tunahitaji kuchukua hatua sawa na hiyo kwasababu wameongoza mauaji ,"alinukuliwa akisema.

Haki miliki ya picha Reuters/AFP
Image caption Doan Thi Huong (kushoto) na Siti Aisyah (kulia) wote wameshtakiwa kwa mauaji ya Bwana Kim

Hata hivyo Bwana Najib baadae alisema marufuku hiyo itawekwa kwa raia wote wa Korea Kaskazini.

Hadi sasa ni watu wawili waliokamatwa na kushtakiwa kwa kuhusiana na mauaji ya Kim Jong nam- mwanamke mmoja wa Indonesia na mwanamke mwingine raia wa Vietnam.

Raia wa Korea Kaskazini aliyekamatwa kuhusiana na mauaji hayo aliachiliwa wiki iliyopita baada ya kukosekana kwa ushahidi dhidi yake, lakini Malaysia inawatafuta watu kadhaa wa Korea Kaskazini , akiwemo afisa mmoja wa kibalozi.

Jumanne, Mkuu wa polisi wa Malaysia Khalid Abu Bakar alisema anaamini wawili miongoni mwa washukiwa wamejificha ndani ya ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Kuala Lumpur.