Mpango mbadala wa Obamacare watangazwa na Republican

Paul Ryan
Maelezo ya picha,

Paul Ryan (pichani) alisema mpango mpya ''utampa kila mMarekani uwezo wa kupata bima ya afya inayofaa na nafuu"

Wajumbe wa Baraza la Congress wa chama cha Republican wametangaza mpango wa afya uliosubiriwa kwa muda kuchukua nafasi ya ule uliosainiwa na rais wa zamani wa Marekani Barack Obama maarufu -Obamacare.

Mapendekezo ya muswada wa sheria hiyo yanatazaiwa kuondoa ahabu kwa waambao hawatanunua bima ya matibabu.

Pia utaondoa mapato yatokanayo na ruzuku ili kupunguza gharama wanazolipia ushuru watu wenye umri mkubwa.

Wajumbe wa chama cha Democrat wamkosoa moja kwa moja mpangu huo, wakisema utakuwa mpango ghali wa huduma ya afya.

Sheria ya malipo nafuu ya bima ya afya, iliyofahamika kama Obamacare, iliwasaidia waMarekani milioni 20 ambao awali hawakuwweza kulipia bima ya matibabu.

Hata hivyo kuongezeka kwa malipo ya bima kumewakera wamarekani wengi.

Maelezo ya picha,

Rais Trump aliuelezea mpango wa bima ya matibabu wa Obamacare, ulioidhinishwa mwaka 2010 na kuonekana kama mafanikio yake ya ndani ya nchi, kama "maafa".

Mpango wa Republicans katika bunge la wawakilishi utapunguza nafasi ya serikali kuu katika kuwasaidia waMarekani kumudu huduma za afya.

"Leo ni siku muhimu katika hatua ya kuelekea kurejeshwa kwa haki ya waMarekani ya kuwa na chaguo na kuwa na uwezo wa kujilipia bima, " Ikulu ya White House ilisema katika taarifa yake

Rais Donald Trump anasubiri kushirikiana na Congresi kurekebisha na kubadili sheria, alisema.

Rais Trump aliuelezea mpango wa bima ya matibabu wa Obamacare, ulioidhinishwa mwaka 2010 na kuonekana kama mafanikio yake ya ndani ya nchi, kama "maafa".

Chama cha Republican kina wingi wa uwakilishi katika mabunge yote mawili , lakini bado kuna mgawanyiko juu ya upi unaopaswa kuwa mpango mbadala wa bima ya afya utakaokuwa nafuu kwa waMarekani utakaopendwa na majimbo mengi yakiwemo yale yanayoongozwa na Republican.