Msanii achora picha ya Beyonce kwenye midomo yake

Haki miliki ya picha Instagram
Image caption Msanii achora picha ya Beyonce kwenye midomo yake

Picha ya mwanamuziki Beyonce ambayo inaonyesha ujauzito wake, imesambazwa mara nyingi mitandaoni lakini wakati huu, ndiyo mara ya kwanza imechorwa kwenye midomo ya mtu.

Msanii wa urembo Jazmina Daniel, alifurahishwa na picha hiyo, yenye mashabiki wengi zaidi kwenye mtandao wa Instagram, na ilimchukua zaidi ya masaa manne kuichora kwenye midomo yake.

Alichora picha nzima ya Beyonce na kujumuisha pande zote za picha hiyo ya mwanamuziki huyo mjamzito.

Haki miliki ya picha Instagram
Image caption Picha hii ya Beyonce kwa sasa ina mashabiki milioni 10 kwenye mtandao wa Instagram.

Picha hiyo ya Beyonce kwa sasa ina mashabiki milioni 10 kwenye mtandao wa Instagram.

Aliichapisha mwanzo wa mwezi Februari, alipotangaza kuwa yeye na mumewe Jay Z wanawatarajia watoto mapacha.