Ndovu mkubwa auawa nchini Kenya

Ndovu mkubwa auawa nchini Kenya Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndovu mkubwa auawa nchini Kenya

Mmoja wa ndovu wachache ambaye pia ni mmoja wa ndovu wenye miaka mingi zaidi na wakubwa, alikufa kutokana na kile kinachoshukiwa kuwa jaribio la kumwinda .

Satao II, ndovu mwenye umri wa miaka 50 ambaye pia anafahamika kama "giant tusker", alipatikana akiwa amekufa kwenye mpaka wa mbuga ya kitaifa ya Tsavo.

Watunzi wa wanyama kwenye mbuga hiyo wanaamini kuwa ndovu huyo aliuawa na mshale wenye sumu licha ya kile kilichosabisha kifo chake hakijathibitishwa.

Satao alipewa jina hilo baada ya kuuawa kwa ndovu mwingine mkubwa mwaka 2014.

Kwa sasa kuna ndovu wasiozidi 30 wakubwa ambao wana pembe zinazoweza kufika ardhini.

"Huyu ndiye ndovu ambaye angeonekana kwa urahisi, wengine huwa vigumu kuonekana," alisema mkuu wa ufadhili wa mbuga ya Tsavo Richard Moller.

"Amekumbwa na matatizo mengi kama ukame na majaribio ya kumuaa."

Kundi kutoka kwa mbuga hiyo na shirika la wanyamapori la Kenya, walipata ndovu msoga wa ndovu huyu ukiwa na pembe zake kabla ya wawindaji kukimbia nazo.

Moja ya pembe hizo ilikuwa na uzito wa kilo 51.5 huku nyingini ikiwa na kilo 50.5.