Mahakama yamzuia Malema kuchochea unyakuzi wa ardhi

Julius Malema alinda chama cha ANC baada kutimuliwa kutoka chama cha ANC Haki miliki ya picha AFP
Image caption Julius Malema alinda chama cha ANC baada kutimuliwa kutoka chama cha ANC

Kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) nchini Afrika Kusini Julius Malema, amezuiwa na mahakama kuchochea kutwaliwa kwa ardhi.

Mahakama ya juu mjini Pretoria, ilitoa uamuzi huo baada ya ombi lililowasilishwa na shirika la umma la AfriForum, kumzuia Malema kuchochea unyakuzi wa ardhi.

AfriForum ilialamika kuwa bwana Malema amekuwa akitoa wito kwa watu kunyakua ardhi hata baada ya shirika hilo kupeleka ombi mahakamani imzuie Malema.

Baada ya agizo hilo AfriForum ilisema kuwa ikiwa bwana Malema atatoa wito zaidi atakuwa amekiuka amri ya mahakama.

Chama cha EFF kinasema kuwa sera yake ya kutwaa ardhi ni ya kurekebisha tatizo la kutokuwepo usawa wa umiliki wa ardhi uliochangiwa na ubaguzi wa rangi bila ya kutolewa fidia.

Chama tawala cha ANC nacho pia kinaunga mkono kutwaliwa kwa ardhi lakini kwa kulipa fidia.