Mchoraji mahiri asiyeona nchini Uganda

Huwezi kusikiliza tena
Msanii wa uchoraji

Ritah Kivumbi ni mwanamke mahiri katika tasnia ya Sanaa ya uchoraji nchini Uganda ingawa ni kipofu.

Mwandishi wa BBC Siraj Kalyango alifika katika studio yake ijulikanayo Magezi Art Exbition katika kanisa ya Namirembe mjini Kampala na kujiona jinsi Ritha Kivumbi mchoraji ambaye ana ulemavu wa macho anavyofanya kazi yake.

Image caption Msanii Ritha Kivumba

Ritha alimwambia kuwa ,alipata shida hiyo ya kutoona wakati akiwa mtu mzima, kipindi ambacho alikuwa ameajiriwa kama msimamizi wa nyumba ya sanaa katika chuo kikuu cha Makerere mwaka 2008.

Ilimchukua kipindi cha miaka sita kurudi katika tasnia yake ya sanaa,mara baada ya kugundua kuwa ana uwezo wa kutengeneza hereni.

Image caption Msanii Ritha akiwa ameshika hereni anazotengeneza

Je,msanii huyu huchanya je rangi wakati anachora wakati haoni?

"Kwa sasa nina uelewa wa rangi ninazotaka, uelewa wa rangi hapa ninamaanisha kuwa nikichanganya rangi nyenkundu na njano najua nitapata rangi ya machungwa...na nikitaka rangi ya kijani kibichi najua itanibidi nichanganye rangi ya njano na kijani.

Nina vikopo vyangu ambavyo hutumia huwa naomba msaidizi wangu kunilete vikopo hivyo ambavyo niliweka alama fulani ambazo zinaifahamisha kuwa rangi mbalimbali mfano nikipapasapapasa nitajua kuwa hii ni rangi nyekundu au njano ."

Licha ya msanii huyo kufanya anachoweza na kupenda ili kuweza angalau kijipata kipato lakini anakabiliwa na changamoto mkiwemo hufukuzwa kutoka madukani akiwa anaongozwa na binti yake akiuza michoro yake.

Image caption Msanii Ritha Kivumbi akiwa na rais Mseveni katika picha za magazeti ya Uganda

Pamoja na changamoto nyingi ambazo anazipitia,Ritha anajivunia kazi yake ni fahari Ingawa wakati fulani pesa huwa shida kupatikana lakini anajivunia kazi yake ambayo pia alipewa medali kutoka kwa rais wa nchi hiyo.