Malaysia yaishutumu Korea Kaskazini kukiuka sheria za kimataifa

Image caption Kiongozi wa Korea kaskazini marehemu,kim jong Nam

Waziri mkuu wa Malysia, Najib Razak ameishutumu Korea kaskazini kwa kukiuka sheria za kimataifa baada ya Pyongyang kuzuia raia wa Malaysia kuondoka nchini humo.

Bwana Najib naye haraka aliwazuia raia wa Korea kaskazini kuondoka nchini Malaysia.

Msuguano huu wa kidiplomasia umekuja kutokana na uchunguzi ambao Malaysia unaufanya kuhusu kifo cha kaka wa kambo wa Kiongozi wa Korea kaskazini kim jong Nam, aliyeuawa mjini Kuala lumpur mwezi uliopita.

waziri Razak amesema atafanya kila liwezekanalo kuwalinda raia wa Malaysia

Tangazo hilo limetolewa wakati Polisi wa Malaysia wakisema kuwa raia wawili wa Korea kaskazini wanatafutwa wakihusishwa na mauaji ya dhidi ya Kim jong nam na kuwa wamejificha kwenye ubalozi wa nchi yao mjini Kuala Lumpur.

Khalid Abubakar ni mkuu wa jeshi la Polisi nchini Malaysia

Mkuu huyo wa polisi amerejea kushutumu raia wa Korea kaskazini kutotoa ushirikiano kwa Polisi wanaofanya uchunguzi