Wikileaks: CIA inatumia runinga kupeleleza

Shirika la ujausi cha CIA nchini Marekani Haki miliki ya picha Inpho
Image caption Shirika la ujausi cha CIA nchini Marekani

Mkuu wa kamati ya intelijensia katika bunge la Marekani ametaja kuchapishwa kwa stakabadhi za siri na mtandao wa Wikileaks kuwa kosa baya sana.

Devin Nunes alisema kuwa amekasirishwa sana na uvujaji wa habari uliochapishwa na mtandao huo hiyo jana unaodai kuonyesha vifaa vinavyotumiwa kudukua mitambo ya mawasiliano inayotumiwa na CIA.

Stakabadhi hizo ambazo hazijathibitishwa na makundi huru zinatoa vifaa au programu inayoweza kuchunguza simu za rununu za kisasa, kompyuta au hata runinga.

CIA na Ikulu ya White House zimekataa kusema lolote kuhusiana na mtandao huo.

Haki miliki ya picha Inpho
Image caption Shirika la ujausi cha CIA nchini Marekani

Vifaa hivyo vinavyodaiwa kutumika kama silaha za mtandao vinasemekana kuwa ni pamoja na programu yenye uwezo wa kuchukua ama kuharibu taarifa kwenye kompyuta zenye programu za Windo , Android, iOS, OSX na kompyuta za Linux pamoja na mifumo ya intaneti.

Baadhi ya programu hizo zinaripotiwa kutengenezwa ndani ya nyumba , lakini shirika la Uingereza la Mi5 linasemekana kusaidia kutengeneza nyaya za upelelezi zinazoweza kushambulia televisheni za Samsung.

Msemaji wa CIA hakuweza kuthibitisha taarifa hizi.

"hatutoi kauli juu ya mambo yasiyoaminika ama taarifa za nyaraka zinazodaiwa kuwa ni za ujasusi," alisema.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza hakuweza pia kutoa kauli yake kuhusiana na taarifa hii.

Haki miliki ya picha Huw Evans picture agency
Image caption Mwanzilishi wa mtandao wa Wikileaks Julian Assange

Wikileaks imesema kwamba vyanzo vyake vilishirikisha umma ili kuchochea mjadala juu ya iwapo uwezo wa udukuzi wa CIA ulipita kiwango cha wajibu na mamlaka yake.

Kulingana na mwandishi wa BBC wa maswala ya usalama Gordon Corrora, taarifa hizo za sasa zilizotolewa- zinaonekana kutoa maelzo zaidi ya matumizi ya njia za teknolojia ya kiwango cha juu .

Ni suala la aibu -kwamba shirika ambalo kazi yake ni kuiba siri za watu halijaweza kutunza siri zake lenyewe.

Cororra amesema kuwa kutakuwa na hofu ya kupoteza maeneo ya ujasusi hususan walengwa ambao wanaweza kubadilisha mienendo yao kwasababu sasa wanafahamu nini majasusi wanaweza kufanya.

Halafu kutakuwa na maswali juu ya ikiwa uwezo wa kiufundi wa CIA ulikuwa mpana sana na wa siri.

Kwa sababu nyingi kati ya nyaraka za awali zilielezea uwezo wa CIA wa kulenga vifaa vya wateja, maswali makuu yanaweza zaidi kuwa juu ya nini kinachofahamika kama tatizo la ''usawa''.

Haki miliki ya picha Samsung
Image caption Inadaiwa kuwa wapelelezi hao wamekuwa wakishirikiana na watengenezaji wa tv za Samsung

Hii hutokea pale unapobaini udhaifu katika sehemu ya teknolojia unayotumia, je unawezaje kuweka uwiano juu ya faida ya umma kwa kuwafahamisha watengenezaji wafunge teknolojia yao na kuboresha usalama wa kila mtu kwa faida ya shirika la upelelezi ya kuiacha ili iweze kutumiwa kukusanya taarifa za ujasusi.

Shirika la usalama wa Taifa nchini Marekani (NSA) tayari limekwisha kabiliwa na maswali juu ya ikiwa ina uwiano huu inavyotakikana wakati nyingi kati ya siri zake zilipofichuliwa na Edward Snowden, na sasa huenda ikawa zamu ya CIA .