Mji wa Canada umewaomba radhi wakazi kwa kugawa maji ya waridi

Haki miliki ya picha FACEBOOK
Image caption Chanzo kilikuwa ni kupenya kwa kemikali ya kusafisha maji kwenye mifumo ya usambazaji maji kwa umma

Mji mmoja nchini Canada umeomba radhi baada ya mpango wa kusafisha maji kugeuza maji kuwa rangi ya waridi.

Wakazi wa mji wa Onoway, Alberta, walitoa malalamiko yao kwa ofisi ya mji wakati mabomba yao yalipoanza kutoa maji ya rangi yawaridi siku ya Jumatatu.

Katika kauli yake Meya wa mji huo, Dale Krasnow alisema kuwa hakukuwa na hatari ya madhara ya kiafya lakini mji "ungepaswa kufanya kazi nzuri zaidi ya kuwasiliana na umma juu ya kile kinachoendelea".

Meya huyo alisema kuwa ilikuwa ni athari ambayo ilitokea kwa bahati mbaya wakati wa harakati za kawaida za kusafisha maji kwa kutumia kemikali ya potassium permanganate ambayo hutumiwa kawaida.

Watu sita wauawa msikitini Canada

Mauaji ya wanawake yakithiri Canada

Maji ya kale zaidi yagunduliwa Canada

Kemikali hiyo kwa kawaida hutumiwa kuondoa madini ya chuma na hydrogen sulphide kwenye maji, na ofisi ya mji ilisema kemikali hiyo iliingia kwenye hifadhi wakati mtambo wa kuichanganya maji uliposimama wakati wa "mchakato wa kawaida wa kuchuja, na kusafisha maji".

"hifadhi ya kemikali ilikaushwa, lakini ya kemikali iliweza kiasi iliweza kupenya na kuingia kwenye mifumo ya usambazaji wa maji.

"huku likiwa ni jambo la kutia hofu kuona maji ya waridi yakitoka kwenye mabomba yako, potassium permanganate hutumiwa katika mchakato wa kawaida wa kuondoa madini ya chuma na manganese na wakazi wa mji hawakuwa hatarini."

Kemikali hiyo inaweza kusababisha kuwashwa kwa ngozi ya mwili, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), lakini hakujawa na ripoti za kutokea kwa athari yoyote mbaya.

Malalamiko zaidi yalikuwa ni juu ya kutoarifiwa kuhusu tukio hilo - wakazi walisema waliudhika kwasababu hawakuambiwa ni kwanini maji yalikuwa na rangi ya waridi hadi Jumanne asubuhi.

"tunaweza kujifunza kutokana na hali hii na kuandaa mkakati kwa ajili ya kushughulikia suala kama hili na mawasiliano mazurihali kamahii itakapojitoke," alisema meya.