Wabunge wa Republican wakosoa muswada mbadala wa ObamaCare

Senata Rand Paul Haki miliki ya picha AP
Image caption Senata Rand Paul ali tuma ujumbe wa Twitter: "Kwa kweli hii inaonekana kama Obamacare Lite!"

Muswada mbadala wa Republican uliosubiriwa muda mrefu kuchukua nafasi ya sheria ya rais Barack Obama ya afya unakabiliwa na upinzani kutoka kwa wajumbe wenyewe wa Republican bungeni.

Tume za bunge zinapanga kuanza kupigia kura sheria ambayo itaondoa adhabu kwa wale ambao hawatanunua bima - mnamo Jumatano.

Lakini wabunge wa bunge la congresi wa chama cha Republican wamekuwa wakisema kuwa mpango huo ni mpana lakini si mpana wa kutosha.

Seneta Rand Paul amesema kuwa mswada huo " utakufa pindi utakapowasili'' ndani ya seneti.

Yeye pamoja na wakosoaji wengine wenye itikadi za kihafidhina wameupuuzilia mbali muswada huo wakiutaja kama "Obamacare 2.0" ama "Obamacare ulio Lite ".

Sheria ya matibabu maarufu kama Obamacare, ilisaidia watu milioni 20 ambao awali hawakuwa na bima kupata bima ya matibabu.