Mbadala wa Obamacare bado wapingwa

Image caption Paul Ryan,Spika wa baraza la wawakilishi

Rais Trump anaendelea kufanya mikutano na wanachama wakuu wa Bunge la Congress ili kuendeleza mpango mpya utakaochukua nafasi ya Obamacare,bima iliyoanzishwa na mtangulizi wake Barack Obama. Sheria hiyo mpya imepingwa na Wabunge kutoka pande zote na imedaiwa kuwa bima hiyo mpya itawaacha Wamarekani wengi bila huduma hiyo.

Huku Spika wa baraza la wawakilishi, Paul Ryan akiunga mkono muswada huo, akieleza kuwa muswada huo ni wenye kusisimua, utakaorejesha mamlaka kwa madaktari, wagonjwa na serikali. Mpango mpya unaweza kubakiza baadhi ya vipengele vya sheria ya sasa lakini utakata ruzuku. Lakini kumekuwapo na mapingamizi kutoka katika chama cha Donald Trump baadhi wakidai mabadiliko yameenda mbali sana na wengine wakisema hayajaleta mabadiliko ya kutosha.