CIA lasema Wikileaks unahatarisha maisha ya Wamarekani

Shirika la ujasusi nchini Marekani CIA
Image caption Shirika la ujasusi nchini Marekani CIA

Shirika la ujasusi nchini Marekani limeushutumu mtandao wa Wikileaks kwa kuhatarisha maisha ya Wamarekani kupitia kuchapisha kile mtandao huo unasema ni vifaa vya kisiri vinavyotumiwa na shirika hilo kupata habari.

Katika taarifa, shirika la CIA halijathibitisha uhakiki wa nakala hizo lakini linasema kuwa raia wa Marekani wanafaa kuwa na wasiwasi na ufichuzi huo.

Shirika hilo limesema kuwa ufichuzi huo hauhatarishi raia wa taifa hilo na operesheni zake bali linawapatia maadui wa taifa hilo vifaa vya kudhuru taifa hilo.