Trump afanya mikutano ya kuondoa ObamaCare

Rais Donald Trump wa Marekani
Image caption Rais Donald Trump wa Marekani

Rais wa Marekani Donald Trump anaendelea kufanya mikutano na maafisa wa vyeo vya juu katika Bunge la Congress anapojitahidi kuwasilisha na kisha kuwashawishi wabunge kupiga kura kuunga mkono mpango wake wa bima ya afya kuchukua nafasi ya bima iliyobuniwa na mwanzilishi wake.

Pendekezo hilo la Bwana Trump limepingwa na watu kutoka pande zote.

Waliopinga hivi karibuni zaidi ni madaktari wanaosema watu wengi wa mapato ya chini watabakia bila bima ya afya.

Ingawa chama cha Bwana Trump cha Republican kinathibti mabunge yote mawili ya Congress huenda asipate idadi ya wabunge watakaomuunga mkono.

Wanachama wa Democrats wameonya dhidi ya kuharakisha upitishaji wa mswada huo katika Bunge la Congress, lakini baadhi ya viongozi wa Republican wanasema wanataka mswada huo utiwe sahihi kabla ya sikukuu ya Pasaka.

Aprili mwaka uliopita bima inayojulikana kama Obamacare ilisaidia kuwalipia huduma za afya zaidi ya watu milioni 20 ambao hawana bima ya afya.