Justin Bieber bandia ashtakiwa kwa makosa 900

Justin Bieber akitumbuiza katika tamasha 2016 Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Justin Bieber akitumbuiza katika tamasha 2016

.Mwanamume mmoja nchini Australia aliyejisingizia kuwa mwimbaji Justin Bieber na kutafuta picha za watoto za aibu ameshtakiwa kwa makosa 900 ya kuwadhalalisha watoto

Inadaiwa kuwa mtu huyo mwenye umri wa miaka 42 alitumia mitandao ya kijamii kuwasiliana na watoto hao.

Awali alikuwa ameshtakiwa kwa kuwa na vifaa vya kuwadhalalisha watoto na uchunguzi zaidi ulisababisha mtu huyo kushtakiwa kwa makosa na ubakaji na kuwatumia watoto vibaya.

Polisi walisema kwa kuwa watoto wengi waliamini kwamba walikuwa wakiongea na Bieber, wazazi wanapaswa kutafuta njia bora zaidi za kuwaelimisha watoto jinsi ya kuwasiliana kupitia mitandao ya kijamii.