Shimo la sungura, lafichua hekalu la miaka 700

Shimo la sungura lililosababisha kupatikana kwa hekalu la miaka 700 Uingereza Haki miliki ya picha Caters
Image caption Shimo la sungura lililosababisha kupatikana kwa hekalu la miaka 700 Uingereza

Mashimo ya kipekee ya sungura katika shamba yameenea hadi kwenye eneo la chini ya ardhi la ibada linalosemekana kuwa lilitumiwa kwa ibada za viongozi wa dini wa zama za kale.

Kwa mujibu wa mkazi wa eneo hilo, mapango ya Caynton , yaliopo karibu na Shifnal, katika Shropshire, yalikuwa yakitumiwa na wafuasi wa madhehebu yaliyokuwa yakiendesha ibada za usiku katika karne ya 17.

Yakiwa chini ya kina cha mita moja kwenda ardhini , mashimo hayo yanaonekana kuwa ni mahali pasipoguswa.

Haki miliki ya picha caters
Image caption caters

Madhumuni yake ya awali yalikuwa ni kuwazika watu, lakini taasisi ya kihistoria ya Uingereza inayoyaelezea mahandaki hayo kama "grotto", inaamini huenda yalijengwa katika karne ya 18 ama nyuma kidogo ya karne ya 19 - miaka mia moja baada ya kuvunjwa kwa maeneo ya zamani ya ibada.

Katika ripoti yake, taasisi hiyo inasema mapango hayo yanaonekana kuwa yalitumiwa kwa "uchawi " na watu walioyatembelea.

Haki miliki ya picha caters
Image caption caters

Michael Scott, kutoka Birmingham, alikwenda kuyapiga picha mapango hayo baada ya kuona video yake kwenye mtandao.

Alisema: "nilitembea kwa wasiwasi kwenye uwanja kuyatafuta, lakini kama hukufahamu kama mapango yako mahali hapo ungeliweza kuyapita.

Ukizingatia muda pango hilo limekuwepo ni hali ya kufurahisha, ni kama hekalu la chini ya ardhi."

Haki miliki ya picha caters
Image caption caters

Njia ya chini ya ardhi inaelekea kwenye mtandao wa njia na majivu yaliyochanganywa na mchanga wa mawe, kijiwe cha kuweka maji ya baraka.

"ilibidi nichechemee na wakati mmoja kulikuwa kimya kabisaa. Kulikuwa na buibui wachache mle ndani basi. Mvua ilikuwa inanyesha kwa hiyo njia ya kuelekea huko ilikuwa inateleza lakini ndani ya pango kulikuwa kukavu," alisema Michael Scott.

Mjusi anayebambua magamba yake kuepuka adui

Mapango hayo yaliripotiwa kuzibwa hadi mwaka 2012 kwa ajili ya kuzuwia wizi na watu wanaofanya "uchawi ".

Haki miliki ya picha caters
Image caption caters

Waliokuwa wakifanya maombi kwenye hekalu hizo ni wanajeshi wa zamani wa kikatoliki waliohudumu katika karne ya 12th kulinda maeneo ya hija wakati walipokuwa njiani katika barabara hatari za kuelekea Jerusalemu.

Askari hao walikuwa wakijihami kikamilifu kama jeshi la usiku ambao sheria fulani zilikuwa zikiwapendelea na hadhi yao ilikuwa ikilindwa na kanisa. Waliheshimiwa kama watu wenye utajiri mkubwa na mamlaka.

Haki miliki ya picha caters
Image caption Mtawa

Mnamo mwaka 1095, Papa Urban II aliahidi kuwapatia msamaha wa dhambi wanaoabudu usiku ikiwa watashiriki vita vya kidini vya kuirejesha Jerusalem katika Ukristo.

Wengi waliitikia wito huo kwa "kuubeba msalaba" na kuonyesha tendo hilo kwa kukata misalaba myekundu kabla ya kuishona kwenye kanzu zao.