UN: Viongozi ndio wa kulaumiwa kwa masaibu Sudan Kusini

Viongozi ndio wa kulaumiwa kwa masaibu Sudan Kusini Haki miliki ya picha AP
Image caption Viongozi ndio wa kulaumiwa kwa masaibu Sudan Kusini

Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini amesema kuwa viongozi wa nchi hiyo wameshindwa kuwatendea haki watu wao na wametelekeza majukumu yao.

David Shearer anasema kuwa wanasiasa wanajali zaidi maslahi yao, kuliko kuhakikisha kuwa chakula na huduma za afya vimewafikia watu wanaokumbwa na njaa na vita vya weyewe wa wenyewe.

Ameongeza kuwa bila ya uwepo msaada ya kimataifa maelfu ya watu nchini Sudan kusini watakuwa wamekufa.

Lakini bwana Shearer alirejelea kile katibu mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa alikuwa amesema Jumatano, kuwa licha ya kuwepo mapigano ya kikabila hakuna dalili ya kutokea mauaji ya halaiki.

Serikali ya Sudan Kusini iliongeza gharama ya kupata stakabadhia za kufaya kazi kwa raia wa kigeni kutoka dola 100 hadi dola 10,000.

Jeshi nalo likanakana kuwa raia wamekuwa wakilengwa kwenye mzozo huo.