Hospitali zaanza kuwafuta kazi madaktari Kenya

Madaktari wamekuwa kwenye mgomo kwa siku 95 nchini Kenya. Haki miliki ya picha AP
Image caption Madaktari wamekuwa kwenye mgomo kwa siku 95 nchini Kenya.

Hospitali nchini Kenya zimeanza kuwafuta kazi madaktari wanaogoma na kuwaondoa kutoka wa nyumba zao.

Huduma kwenye hospitali za umma zimetatizika kutokana mgomo ambao ulianza mwezi Disemba, huku madaktari na wahudumu wengine wa afya wakitaka mshahara zaidi na mazingira bora ya kufanya kazi.

Lakini hatua hiyo ya kuwafuta kazi madaktari inakuja wakati chama cha madaktari kinasema kuwa kimetia sahihi nyaraka zinazohitajika ili kumaliza mgomo wao.

Madaktari nao wanaitaka serikai kufanya hivyo.

Lakini serikali inasema kuwa siku ya mwisho ya kukubali asilimia 50 ya nyongeza ya mshahara ilipita siku mbili zilizopita.

Sasa hospitali zimeanza kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya madaktari ambao wamekuwa kwenye mgomo kwa siku 95.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii