Wafanyakazi wa UN raia wa Malaysia waliozuiliwa Korea Kaskazini wandoka

Kuuawa wa Kim Jong-nam kumezorotesha uhusiano kati ya Malaysia na Korea Kaskazini Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Kuuawa wa Kim Jong-nam kumezorotesha uhusiano kati ya Malaysia na Korea Kaskazini

Wafanyakazi wawili wa Umoja wa Mataifa ambao ni miongoni mwa raia wa Malaysia 11 waliozuiwa kuondoka Korea Kaskazini sasa wameondoka nchini humo.

Wawili hao wanaoajiriwa na shirika la mpnago wa chakula duniani (WFP) waliwasili mjini Beijing leo Alhamisi.

Korea Kaskazini na Malaysia siku ya Jumanne zote ziliwapiga marufuku raia wa nchi zao kuondoka kufuatia mzozo unahusu kuuawa kwa ndugu wa kambo wa kiongzoi wa Korea Kaskazini.

Kim Jong-nam aliuawa na kemikali mbaya kwenye uwanja wa ndege wa Kuala Lumpur.

Malaysia haijailaumu Korea Kaskazini moja kwa moja kwa hilo lakini kuna uvumi kuwa Korea Kaskazini ilihusika.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kim Jong-nam aliomba msaada kwenye uwanja wa ndege muda mfupi kabla ya kushambuliwa kemikali

Wachunguzi wameitaka Korea Kaskazini kusalimisha washukiwa watatu ambao wanaaminiwa kijificha ndani ya ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Malaysia.

Korea Kaskazini imekana vikali kuhusika na mauaji hayo ni kuhusu ni nani anastahili kudai mwili wa Kim.

Katika taarifa fupi WFP ilithibitisha kuwa wafanyakazi wao sasa wako China.

"Wafanyakazi hao ni wa kimataifa na sio waakilishi wa nchi zao," WFP ilisema.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Video ya mtoto wa Kim imeibuka