Jammeh: Nitarudi Gambia kufanya ukulima

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Jammeh asema atarudi Gambia kufanya ukulima

Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh amefichua mpango ya kufanya ukulima kwa mujibu wa gazeti la Jeune Afrique.

Bwana Jammeh alikimbilia Equatorial Guinea mwezi uliopita, baada ya kukabiliana na shinikizo kutoka kwa majirani wa Gambia ambao walitisha kumuondoa madarakani ikiwa hangekubali kushindwa kwenye uchaguzi wa Disemba.

Baada ya kukubali kushindwa, na kisha kukataa kuacha madaraka kwa Adama Barrow, bwana Jammeh alikuwa amesema kuwa angerudi kwao kijijini nchini Gambia kufanya ukulima.